Posts

Showing posts from February, 2024

Ugiriki yahalalisha ndoa za jinsia moja

Image
  Wapenzi wa jinsia moja sasa pia wataruhusiwa kisheria kuasili watoto baada ya kura ya Alhamisi ya 176-76 bungeni. Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis alisema sheria hiyo mpya "itakomesha kwa ujasiri ukosefu mkubwa wa usawa". Lakini imegawanya nchi, kwa upinzani mkali unaoongozwa na Kanisa la Othodoksi lenye nguvu. Wafuasi wake walifanya maandamano mjini Athens. Wengi walionyesha mabango, walishikilia misalaba, walisoma sala na kuimba vifungu vya Biblia katika Syntagma Square katika mjii mkuu . Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi, Askofu Mkuu Ieronymos, alisema hatua hiyo "itaharibu mshikamano wa kijamii wa nchi hiyo". Mswada huo ulihitaji wingi wa kura ili kupitishwa katika bunge hilo lenye wabunge 300. Bw Mitsotakis alikuwa ameunga mkono mswada huo lakini akahitaji kuungwa mkono na vyama vya upinzani ili kuupitisha , huku wabunge kadhaa wa chama chake cha mrengo wa kulia wakipinga.

WASIFU WA HAYATI EDWARD LOWASSA

Image
Wasifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Lowassa by Mzuri Jumaa Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 katika Kijiji cha Ngarash, Monduli akiwa mtoto mkubwa wa kiume kwa Mzee Ngoyai Lowassa na kuanza masomo yake katika Shule ya Msingi Monduli kati ya mwaka 1961–1967. Kisha akaendelea kwenye Shule ya Sekondari Arusha kwa kidato cha Kwanza mpaka cha nne kati ya mwaka 1968 – 1971, na kisha kumalizia kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Milambo mkoani Tabora. Alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974 hadi mwaka 1977 na kuhitimu Shahada ya Sanaa katika Elimu (B.A Education) na baadaye Chuo Kikuu cha Bath, Uingereza kwa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Maendeleo. Baada ya kumaliza chuo kikuu, Lowassa alifanya kazi ndani ya CCM akiwa afisa wa ngazi ya juu kuanzia wilaya, mkoa na baadaye makao makuu kati ya mwaka 1977 hadi mwaka 1989. Lowassa aliwahi pia kutumikia jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzani...